GET /api/v0.1/hansard/entries/1024846/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1024846,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1024846/?format=api",
"text_counter": 504,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Zani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13119,
"legal_name": "Agnes Zani",
"slug": "agnes-zani"
},
"content": "Bi Naibu Spika, asante kwa fursa hii ili nizungumzie juu ya Ombi kutoka kwa watu wa Jomvu, Mombasa. Nakushukuru Sen. Faki kwa kuleta Ombi hili hapa Seneti. Kwa kweli vile alivyosema na vile ambavyo tumeona, haya maombi ni juu ya dhulma ya kihistoria. Hawa ni watu ambao walikuwa na ardhi yao na walikuwa wakifanya shughuli zao na mambo yao ya kila siku. Lakini, inaonekana kwamba hapa kati kati mambo yaligeuka. Inaonekana kwamba sasa hawawezi kuimiliki hiyo ardhi vizuri na wametupwa nje. Ninafikiria kwamba kwa sababu wameleta Ombi hili hapa Seneti, Kamati husika ina kazi ya kuangalia jambo gani haswa lilifanyika. Kwa upande wangu, sio vibaya kutoa ardhi kwa kanisa, lakini nimemuuliza Sen. Faki akaniambia ni karibu ekari 150 ambayo inahusika. Ekari hizi pia zinauzwa kwa watu wengine sasa. Wale watu ambao walikuwa wakiishi pale tangu zamazi sasa hawapati nafasi. Wanaamini kwamba hii ni ardhi ya ukoo. Bi Naibu Spika, ni ardhi ambayo wameimiliki kwa miaka mingi sana na wanahitaji kama ni kwa upande wa uchumi, kufanya biashara, ukulima na chochote na ardhi ile. Kwa sababu wameona kwamba dhulma hii imeendelea, na haswa katika Pwani tumeona dhulma nyingi sana kwa upande wa ardhi, hawa watu wa Jomvu wanaoleta Ombi hili katika Seneti wameleta mahali sawa. Hili Ombi ni muhimu. Nafikiria ikienda kwa Kamati hii itashughulikiwa na wataweza kutuelezea ni haswa jambo gani. Nafikiria wengine pia wataitwa hapa Seneti ili waweze kujielezea zaidi ili tupate kujua haswa ni kitu gani kilifanyika ili tuweze kutatua shida hiyo. Bi Naibu Spika, kama hii ardhi ilipatiwa kanisa kwa sababu ya kazi fulani, basi sio ardhi yote, kama wale ambao ni wakaazi pale hawajapata chochote. Itabidi maswala haya yangaliwe. Vyeti vya kumiliki ardhi pia viangaliwe kwa njia ambayo itaweza kusaidia kujuwa kwamba ardhi ilikuwa ni ya nani na ardhi inapaswa iwe na nani. Hili swala la kuuza ardhi ni muhimu sana kutoka Pwani. Hii kwa sababu tunaona kwamba ardhi nyingi zikiuzwa, wale ambao walikuwa wakimiliki ardhi hizo wanapata kwamba hawana mahali pa kuenda. Ikiwa humiliki ardhi ya babu na nyanya zako wa zamani, itakuwaje sasa na utaishi wapi."
}