GET /api/v0.1/hansard/entries/1024850/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1024850,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1024850/?format=api",
"text_counter": 508,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13200,
"legal_name": "Issa Juma Boy",
"slug": "issa-juma-boy"
},
"content": "Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia. Kwanza, nataka kumpongeza Bw. Salim Mwidali, mkaazi wa Jomvu, kwa kuleta hii Petition katika Seneti. Bi. Naibu Spika, kama unavyojua, ardhi ni jambo sugu sana katika nchi hii. Kila unapokwenda, tatizo kubwa ni ardhi. Ukienda Mombasa, sehemu za Bonde la Ufa na sehemu zingine, shida kubwa utaona kwamba kuna unyanyasaji wa ardhi katika nchi hii yetu. Kusema ukweli, mimi mwenyewe nikiwa mdogo, historia ya Jomvu tuliisoma katika vitabu vya historia ya Kenya. Inajulikana kuwa Jomvu iko sehemu gani na Jomvu ni pahali gani. Ni pahali ambapo katika historia, inajulikana sana. Jomvu ni mji wa zamani sana. Mji huu una historia ya biashara. Bi. Naibu Spika, kusema ukweli, haki lazima ifuatiliwe. Sisi kama viongozi lazima pia tuweze kuchangia. Hii ni kwa sababu malalamikio haya yapelekwa katika National Land Commission (NLC) katika nchi yetu ya Kenya. Utakuta kwamba, kesi nyingi zikienda katika tume hii hawachukui jukumu la haraka kutatua tatizo hili ya ardhi. Wao wanasikiza malalamiko ya wananchi lakini haki na utendaji wa haki hazifuatiliwi. Bi. Naibu Spika, haki katika ardhi hii lazima ifuatiliwe. Kama kuna kamati itachunguza hii ardhi ya watu wa Jomvu, basi wakae chini na wananchi wenyewe ili waweze kutatua tatizo hili sugu la ardhi. Tatizo hili si la Jomvu pekee yake, bali katika Kaunti ya Kwale. Wakati huu kuna shida ya kule Ramisi ambayo imenyakuliwa na mabepari. Kila siku kuna maandamano. Maandamano hayo utakuta ni mambo ya ardhi pekee yake. Huko sehemu za Waa, Galu na Kinondo, matatizo ni hayo hayo. Bi. Naibu Spika, mimi naomba kwamba hiyo Kamati ambayo itaangalia shida hii, iweze kufanya haki ili watu wa Jomvu wapate haki yako."
}