GET /api/v0.1/hansard/entries/1025282/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1025282,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1025282/?format=api",
"text_counter": 329,
"type": "speech",
"speaker_name": "Trans Nzoia, CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Janet Nangabo",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": " Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuongelea juu y hii ripoti kutoka kwa kamati ya mazingira katika Bunge letu. Ninaungana na wenzangu kushukuru kamati hii. Imekuwa muda haya mambo ya mabwawa yameleta utata mno. Isingelikuwa ni hii kamati imechukua hiyo nafasi, hatungejua kinachoendelea kuhusu mabwawa haya. Nataka kuungana na wale wamesema kwamba haya mambo ya mabwawa yalikuwa chini ya Kamati ya Kilimo. Ni ukweli hatungejua ni nini kinaendelea. Namshukuru Mwenyekiti na timu yake kwa kutambua kwamba hizi shida zenye Wabunge wametambua katika Bunge hili ni kweli ni shida zile ziko kule chini na haikuwa ni makosa ya wale walikuwa wanauliza bali ni makosa ya mipangilio sambamba kuhusu haya mambo ya mabwawa. Umesikia kule Budalang’i vile wamesema. Ni ukweli tusipo kuwa na wataalamu wakutambua kwamba hili bwawa linatakikana litoke wapi na liende wapi tutakuwa tunamaliza wakati wetu an hizo pesa zinatakikana kutolewa na serikali zitakuwa zinaangulia patupu. Ukiona sehemu za Turkana mahali ambapo wanasema ni sehemu kame... Iwapo mtu atapewa kandarasi ya kuchimba kisima au bwawa katika eneo hilo pasipo na ujuzi tutakuwa tunamaliza wakati wetu. Ninamushukuru Mhe. Chachu. Amesema hapa kwamba kuna wale ambao walikuwa wamepewa fedha za kutengeneza bwawa. Unaona mtu akikula karibu asilimia sabini bila kufanya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}