GET /api/v0.1/hansard/entries/1025436/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1025436,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1025436/?format=api",
    "text_counter": 132,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": ". Walitoa ripoti halafu wakaipa Kamati ya Utekelezaji, ama Committee on Implementation, kuhakikisha kuwa yale mambo waliyoambia Kampuni ifanye yanafanywa. Lakini tukaenda kupiga kura mwaka wa 2017. Bahati nzuri nikarudi kwenye Bunge la 12 na nikafufua tena Ripoti hiyo. Kamati ya Utekelezaji ikaanza kuita mikutano ya wahusika kuwahoji hapa Nairobi. Hawakurithika na majibu hayo na wakaamua kuenda Kaunti ya Kwale tarehe 29, mwezi wa tatu, mwaka jana. Saa ni mwaka mmoja tangu Kamati ya Utekelezaji ifike Kwale kwenda kuangalia hali ya wafanyikazi. Hadi leo, bado ripoti haijafika hapa Bungeni licha ya kuwa nimeshafuata viongozi wa Kamati hiyo mara kwa mara kuwaulizia kuhusu Ripoti hiyo. Nimeambiwa kuwa kwa sababu ya ugonjwa wa Covid-19, Kamati haijaweza kukutana. Lakini mwaka mmoja kabla ya Coronavirus kufika Kenya ndiyo Kamati ilienda Kwale kuchunguza zaidi na hadi leo sijapata jibu mwafaka. Nimekuwa na subra sana lakini leo nimeona huenda pia tukaongeza muda mwingine mpaka mwisho ama ikaja Bunge lingine. Kwa hivyo, naomba unisaidie kwa jambo hili. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}