GET /api/v0.1/hansard/entries/1026709/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1026709,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1026709/?format=api",
    "text_counter": 425,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Laikipia CWR, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Catherine Waruguru",
    "speaker": {
        "id": 13253,
        "legal_name": "Catherine Wanjiku Waruguru",
        "slug": "catherine-wanjiku-waruguru"
    },
    "content": " Asante, Naibu Spika wa Muda. Nataka kujipa challenge ya kuzungumza kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu ni moja ya zile lugha ambazo zinatumika pale nje. Naomba kwanza kumpongeza dadangu Bi Gladys Wanga kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuiiongoza Kamati hii inayoshughulikia mambo ya fedha nchini. Heko kwake na kwa wanawake wote ambao wako katika Bunge hii. Handshake inataka nchi ambayo imeungana. Akina mama hatutabaki nyuma pamoja na vijana na walemavu ambao wako katika Bunge hii. Nimesimama kama Mwanakamati wa Kamati hii. Naunga mkono Mswada huu wa kutekeleza Public Finance Management Act ili tuweze kushughulikia Bajeti ama pesa ambazo Rais wa Taifa la Kenya alitangaza ni za kusaidia Wakenya dhidi ya makali ya ugonjwa wa Covid- 19. Maswali mengi yameulizwa kule nje. Wengi wanasema kwamba sisi tulio ndani ya ofisi tunakula pesa. Wengine wanasema pesa hizi hazipatikani kule mashinani. Nashukuru kwa sababu Kamati hii imetupa nafasi ya kujadili jinsi ambavyo hizi shilingi bilioni tatu zitaweza kufika mashinani kwa wafanyi biashara na wachuuzi wadogo wadogo. Naunga usemi kuwa mpango wa kudhamini mkopo kwa wachuuzi wadogo wadogo upite wakati wa Mswada Kusomwa Mara ya Pili. Tukiendelea, tutafanya majadiliano kuona ni jinsi gani hatutarudia yale makosa ambayo yamefanywa na hifadhi zile zingine. Nimeona tabia ya wenzetu katika ule mkono mwingine wa Serikali. Kweli kabisa, wanafanya kazi na kamishna wa kaunti. Lakini wakati mwingine unapata kwamba kamishna wa kaunti anapuuza Wabunge na wale viongozi ambao wamechaguliwa. Hatutaki kuona “ugonjwa” huo kwa pesa ambazo zinasaidia watu kukabili makali ya janga la Covid-19. Kwa hivyo, ile taratibu ambayo inatumiwa iwe kana kwamba inammulika kila mwananchi katika eneo lake la bunge ama eneo lake la kaunti. Lakini hatutaki ikae ni kama pesa hizo ziko kwa “hewa” na zinatumika katika ofisi na sisi tuliochaguliwa hatuhusishwi katika majadiliano. Wananchi wetu wamezoea tabia ya Harambee. Kwa mara ya kwanza, Serikali imekubali kumsimamia mwananchi wa kawaida kuchukua mkopo bila makali ya riba ambayo imekuwa ikiwekwa na benki zetu. Benki haziwaamini wale wachuuzi wadogo. Rais alipofunga nchi, benki zilisema kwamba hazitatuongezea riba. Zimekataa kuwekeza pesa zao kwa mwananchi wa kawaida ila zinazipeleka katika Benki Kuu ya Taifa la Kenya ambapo zitapata returns za juu. Hiyo inafanya mama ambaye anauza mitumba katika soko kule Nanyuki ama Nyahururu kutoweza kupata mdhamini ambaye atamsimamia ili aweze kupata pesa katika benki. Tiba ndio hii. Pesa ndizo hizi - shilingi bilioni tatu ambazo Rais alipatiana. Zitawezaje kufika kwa mifuko yetu bila kudaiwa na zile factors ambazo zimezuilia Uwezo Fund na Youth Fund kufika kule mashinani? Tunataka kuona yule waziri anayehusika akifanya kazi na Wabunge waliochaguliwa. Tunataka kuona Wabunge wa kike wamechaguliwa na pesa hizo zifike kule mashinani ili ripoti itakayoletwa isiseme kwamba ni watu wa Nairobi ama watu ambao wanakaa katika miji ambao wanafaidika. Ndio maana unapata kuwa Kazi Mtaani inahusisha wale watu wako katika maeneo"
}