GET /api/v0.1/hansard/entries/1027148/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1027148,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1027148/?format=api",
"text_counter": 337,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika, taratibu tunazoziona mbele yetu hivi sasa ni aibu katika Bunge letu la Seneti. Hatujawahi kuwa na hali kama hii katika miaka minane ambayo nimekuwa Seneta. Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu ya Kenya, tunataka kuigawanya Kenya yetu. Kenya ni nchi moja na sisi wote ni wakenya. Mwenendo ambao tunataka kuchukua, utaleta shida baada ya miaka miwili. Tarabitu inayopendekezwa italazimu wengine wetu kubeba mabango baada ya miaka miwili kusema kwamba ‘Pwani si Kenya’. Nasema hivyo kwa sababu sehemu za Pwani zimelaliwa sana. Sehemu za Kaskazini Mashariki pia zimelaliwa sana. Sehemu ambazo wanatoka ndugu zetu wa North Eastern, Maasai na Ukambani zimelaliwa sana kwa ugavi wa pesa tangu uhuru upatikane. Tumeahidiwa lakini bado tunarejea pale pale. Tunaambiwa eti, ‘ndugu zetu, pigeni tick . Tutawapa miaka miwili mufaidike kidogo lakini hamtakuwa Kenya baada ya miaka mitano.’ Ni lazima tutafakari swala la uteti kama huu ndiposa tusipasue nchi mara mbili. Hii ni kwa sababu tunataka Kenya yetu iwe nchi moja. Hili swala la kupitisha ugavi kwa miaka miwili ni kama kupea mtu ambaye anaugua cancer ama maradhi fulani Panadol badala ya kumpea dawa ama shindano zinazotakikana kutibu ule ugonjwa. Kuhairisha hii ni kukosa kutibu ule ugonjwa. Tukitaka kutibu huu ugonjwa, ni lazima tuitibu na taratibu za hesabu ili kila kaunti ya Kenya ifaidike saa hizi na sio baadaye. Kila mtu atakwenda nyumbani ikiwa ugavi wa pesa hizi utakuwa uko sawasawa na hiyo ndiyo ukamilifu kama sote tuko wakenya. Hatutaki kukubali kisha tuanze kugombana na kuleta fujo, ghasia na aibu katika bunge la Seneti kama vile tunavyo iona hivi sasa baada ya miaka miwili."
}