GET /api/v0.1/hansard/entries/1028026/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1028026,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1028026/?format=api",
"text_counter": 62,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "shamba. Ni haki ya wananchi kuishi katika hali ya kuheshimika. Kuna IDPs wengi mahali pengi, wanaishi katika hali ya uchochole, na hawana mashamba. Ninajua hili Ombi litaenda kwa Kamati yangu ya Mashamba, Mazingira, na Rasilmali Asili, na tutalivalia njuga swala hili ili tuangalie wananchi ambao hawana mashamba katika sehemu tofauti za Kenya, na tusukume Serikali kuwapa mashamba. Wakati mwingine Kamati ya Mashamba, Mazingira na Rasilmali Asili tulienda hadi kuangalia wananchi waliofukuzwa kutoka Msitu wa Marmanet, walitupwa barabarani na wanaishi katika hali mbaya sana. Hali tuliyoona pale ilikuwa ya kuhuzunisha ajabu. Ajabu ni kwamba, mpaka sasa, wale watu bado wanaishi katika ile hali. Hawajapewa mashamba, na kuna mashamba mengi sana Kenya yanayoitwa"
}