GET /api/v0.1/hansard/entries/1028028/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1028028,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1028028/?format=api",
"text_counter": 64,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Ni jukumu la Serikali kufunga buti na Wizara ya Mazingira na Misitu, na National Land Commission (NLC) kuwapatia wananchi hao mashamba yao. Nikimalizia, ningependa kuongelea umuhimu wa kuangalia mambo ya Maombi. Kule Taita Taveta, kuna wananchi waoishi sehemu ya Mwakitau ambao walileta Ombi kwa Bunge hili. Serikali ya Kenya itoa title deed kwa ranch na wananchi zaidi ya 10,000 saa hizi wanafukuzwa kutoka kwa hiyo ranch kwa sababu title deed ilipewa ranch mwaka wa 1985, na hao wananchi walianza kuishi hapo mwaka wa 1919, wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia. Walipagana huko na wakafanya makaazi hapo. Hii Petition bado haijamaliziwa na korti imepeana hadi mwezi wa kumi watu hao watolewe kwa hiyo ardhi. Naomba kuwa wakati tunaangalia haya maombi mengine, na Mwenyekiti wangu yuko hapa, tuangalie zile Petitions zingine ambazo hazijaangaliwa pia ili wananchi wetu wa Kenya waishi katika amani. Singependa kusema zaidi ya hapo, ila kushukuru Wakenya kwa sababu ya ile imani walio nayo na Bunge la Seneti, kwamba wakileta matataizo yao hapa, yanaangaliwa kwa haraka. Asante."
}