GET /api/v0.1/hansard/entries/1028168/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1028168,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1028168/?format=api",
"text_counter": 204,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "kwamba wengi wa wale wagonjwa itawabidi waje Nairobi ili waweze kupata matibabu ya ICU kama hayo. Ni muhimu kaunti zetu zijitayarishe na vitanda kama hivyo. Watu wengi wanaondoka kutoka mji wa Nairobi na Mombasa kwenda mashambani. Baadhi yao wanapeleka ugonjwa kule mashambani. Hii ni hatari ambayo itakumba nchi yetu iwapo vitanda kama hivi havitakuwa katika sehemu nyingi za kaunti zetu. Pia, tumeona watu wamepumua au kurelax, kwa lugha ya Kiingereza, katika kupambana na janga hili la COVID-19. Utaona kwamba watu wengi mjini wanatembea bila barakoa, wengine hawaoshi mikono na hawatumii sanitizers. Hivi ni vitu ambavyo vilikuwa vinahubiriwa kwa muda mrefu kabla ya kurelax masharti haya. Bi. Spika wa Muda, kuna haja ya watu kurejelea katika uhubiri wa haya masharti ili kila mtu ajue kwamba ugonjwa bado upo. Nafasi tu imetolewa lakini ugonjwa bado upo na ugonjwa umekuwa hatari zaidi. Kwa sasa, wale ambao wameathirika na wakaaga ulimwengu hawakuchukua muda wa siku tatu au nne. Kwa siku mbili au tatu waliweza kupoteza maisha."
}