GET /api/v0.1/hansard/entries/1028637/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1028637,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1028637/?format=api",
"text_counter": 302,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Haika Mizighi",
"speaker": {
"id": 13274,
"legal_name": "Lydia Haika Mnene Mizighi",
"slug": "lydia-haika-mnene-mizighi"
},
"content": " Asante sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia hii fursa na pia mimi niweze kuchangia suala hili ambalo linahusu mambo ya usawa wa jinsia na maendeleo. Tunaongea kuhusu jinsia ya kiume na kike. Tunaongea kuhusu maendeleo, afya, ugavi wa kazi, elimu na masuala mengineyo ya kuboresha maisha ya jamii nzima. Tumeona mara nyingi kina mama wakienda barabarani kuitisha haki zao hapa na pale. Tumeona vijana na vile vile watu wanaoishi na ulemavu wakiwa barabarani wakisema, 'Haki yetu, haki yetu!' Haki hii haifai kuombwa bali ni vile wanajisikia wakiwa wamenyanyasika na hawapati hiyo haki yao. Kwa hivyo, kama Hoja hii itaboresha mambo na kuleta mwafaka, basi mimi naunga mkono. Kuna suala la BBI ambalo limetajwa. Mimi bado niko pale pa kusoma. Naendelea kusoma, lakini ni huzuni kwamba nafasi hii ya kiti cha Mwakilishi wa Wanawake ambacho kilinileta hapa Bungeni naona kama tutaenda kukikosa kupitia hii BBI. Bado naendelea kusoma. Asante kwa hii fursa."
}