GET /api/v0.1/hansard/entries/1028829/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1028829,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1028829/?format=api",
    "text_counter": 109,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bi. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyosomwa na Mhe. Spika. Kwanza niruhusu niwape kongole Spika pamoja na Seneti nzima kwa uamuzi wao wa kwenda mahakamani kutetea haki ya kikatiba ya Seneti. Vilevile nawapa kongole mawakili wote ambao walihusika katika kesi hii tukiongozwa na Mhe. Orengo, Mhe. Omogeni, Mhe. Sen. Mutula Kilonzo Jnr. na wale wengine wote ambao tulikuwa nyuma tukitoa mawazo na usaidizi wa aina nyingine. Nilikuwa na Sen. Omogeni wakati kesi ilipokuwa inazungumzwa. Kwa hakika alizungumza kwa ujasiri mkubwa akisaidiana na wakili Bi. Mercy Thanji ambaye yuko katika Idara ya Sheria katika Bunge letu la Seneti. Vilevile ningependa kuipongeza Mahakama kwa kutoa uamuzi ule kwasababu imetoa uamuzi kwa ujasiri ili kuhakikisha kwamba imetangaza kuwa sheria 29 zimepitishwa kinyume cha sheria."
}