GET /api/v0.1/hansard/entries/1028830/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1028830,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1028830/?format=api",
"text_counter": 110,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Wakati huu ambapo tunapongeza Mahakama kuna Majaji 40 ambao wamechaguliwa na Tume ya Kuajiri Mahakimu ambao Mhe. Rais amekataa kuwatangaza rasmi na kuwaapisha kama Majaji. Kitendo hicho kinahujumu Katiba kwasababu JudicialService Commission (JSC) ikipendekeza Majaji waajiriwe, inapendekeza kwasababu imewafanyia ukaguzi na kila kinachotakiwa kufanywa kuhakikisha kwamba wale Majaji wameweza kuchaguliwa. Hatuwezi kupigania uhuru wa Seneti au Seneti iweze kupata nguvu zaidi wakati mahakama inaendelea kuhujumiwa na Rais."
}