GET /api/v0.1/hansard/entries/1028849/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1028849,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1028849/?format=api",
    "text_counter": 129,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Shukran Bi. Naibu Spika. Nataka kuchangia Taarifa iliyosomwa na Spika wetu kuhusiana na kesi iliyokua kortini. Jambo la kwanza ni kuwashukuru Maseneta ambao ni mawakili ambao waliweza kutuwakilisha katika kesi hii, hususan Sen. Orengo, Sen. Omogeni, Sen. Mutula Kilonzo Jnr., na mawakili wengine walioweza kuchangia. La muhimu katika hii ni kwamba tulipokuwa tukipeleka kesi hii Kortini, sote tulikua tumekubaliana kwamba kulikua na dhulma ambayo ilikua imefanywa na hatukupendelea katika zile sheria 24 ambazo zilipitishwa bila kuhusisha Seneti wala Spika wetu kuwa katika mahojiano kama hayo. Kipengele cha 110(3) katika Katiba yetu kiko wazi na kinasema kuwa kabla Bunge letu kukubaliana na Mswada, ni lazima Spika wa Seneti na Spika wa Bunge la Taifa waweze kukaa na kujadiliana kuhusiana na ule Mswada. Wakiona kuwa ni maalum ama ni wa kawaida, wanaweza kuona jinsi ule Mswada utaanza. Jambo la kusikitisha ni kwamba Bunge la Kitaifa limekua likipuuza na hivi sasa imebainika wazi kuwa Seneti ina uwezo katika ile sheria inayosema kuwa hakuna The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}