GET /api/v0.1/hansard/entries/1028850/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1028850,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1028850/?format=api",
"text_counter": 130,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Mswada ambao unaweza kupitishwa bila Seneti kuhusishwa. Ule uerevu waliokua wakifanya, Waswahili husema, “mwerevu hajinyoi.” Hata uwe mwerevu namna gani, huwezi kuchukua makasi ukajinyoa. Sheria kama hii ya kuzembea ama kutotii amri katika Katiba ndio sisi tunasema kwamba Mahakama imefanya jambo la muhimu kuweza kuurekebisha na kuweka sawa. Vile vile, nataka kuwapea kongole Majaji walioketi kusikiza kesi hii. Majaji hao wamefafanua kabisa na kueleza kila kitu kinaga ubaga kwamba, hamtachukua sheria kwenye mikono yenu na kufanya vile mnavyotaka. La mwisho ni kwamba, sisi tukiwa hapa Seneti, tunahitaji Wabunge wa Bunge la Kitaifa waweze kuelewa kwamba Seneti linahitaji kupewa heshima yake. Sheria kama hii ambayo imewekwa hivi sasa, tunatarajia kuwa Spika wetu anajukumika kusimama kidete na hutatingisika. Hata iwe mchana au usiku, utaangalia kwamba haki ya Seneti haikuweza kuzimika."
}