GET /api/v0.1/hansard/entries/1028869/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1028869,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1028869/?format=api",
    "text_counter": 149,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Naibu Spika, ningependa kuchangia Kauli hii na kusema kwamba ni jambo ambalo linapigia upato swala zima la nguvu ya Bunge la Seneti, hususan, uamuzi huu ambao umeweza kutupilia mbali ama kuweka shaka ama dosari Sheria 23 ambazo zimeweza kupitishwa pasipo kuhusisha Seneti. Mwanzo, ninashabikia uamuzi huu kwa sababu tunafaa kukumbuka kwamba hatuna Mabunge mawili. Tuna Bunge moja la Kitaifa ambalo lina nyumba mbili. Nyumba hii ya Bunge la Seneti sio tu Nyumba ya kushughulikia maswala ya ugatuzi, ni kuhakikisha kwamba maswala ya ugatuzi yanawiana na sera ya kitaifa. Mara nyingi, tunaona kwamba kuna kule kutokuelewa kwa nia ya Bunge hili, hususan mkono wa Serikali wa utekelezaji. Watu wengi hawajaweza kutathmini maudhui ya uamuzi huu. Ni kumaanisha kwamba, jukumu la kuonyesha kwamba sheria ama Mswada wowote hauhusiani na maswala ya serikali gatuzi ama kaunti. Jukumu hilo sasa sio la Bunge la Seneti, lipo katika Bunge la Kitaifa. Kwa sababu, kama vile ambavyo korti iliamua, utawezaje kusema kwamba kuna sheria ambazo zinatekelezwa katika Serikali ya Kitaifa pasipo na maeneo ya kaunti? Haiwezekani kwa sababu ukiangalia nchi hii, hata Jiji la Nairobi ni kaunti. Kwa hivyo Bi. Naibu Spika, ningependa kusema kongole na hongera kwa sababu hatukuweza kushtushwa. Hata ilikuwa wakati juzi tu, unaona kama kuna midahalo kwamba tutupilie kesi mbali kwa sababu tunaweza kuwa na udhamini wa miswada kati ya maseneta na wabunge wa Bunge la Kitaifa. Lakini, hiyo sio suluhu. Mimi mwenyewe nimeweza kudhamini zaidi ya miswada mitano katika Bunge hili. Tunafanya kazi nyingi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}