GET /api/v0.1/hansard/entries/1028870/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1028870,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1028870/?format=api",
"text_counter": 150,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13129,
"legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
"slug": "isaac-mwaura"
},
"content": "kama Maseneta lakini, miswada hii hata iwe inaweza kuwasaidia Wakenya, inaweza kufungua masoko yetu yawe huru. Mara nyingi miswada hii haiwezi kupitishwa katika Bunge la Kitaifa ilmradi kwamba inhusisha mambo ya kifedha. Mhe. Naibu Spika, ninafikiri ni jambo ambalo tunafaa kuliangalia kwa undani, tuweze kuona sisi ambao tuko hapa, swala hili zima lisiweze kutumiwa kuweza kudhoofisha nguvu za Seneti katika mchakato wa Building Bridges Initiative (BBI) . Tuchukue hii nafasi tuseme kwamba tufuatilie na huu uamuzi, kwa sababu, nimeona katika vyombo vya habari kwamba Bunge la Kitaifa limeweza kusema kwamba litakata rufaa uamuzi huu. Tuhakikishe kwamba, kama vile tumetoka kule Naivasha kwamba vipengele hususan ambavyo vinahusikana na ugavi wa fedha kati ya Serikali ya kitaifa na serikali gatuzi zozote, isiwe kwamba sasa hivi hatuna ushawishi. Kwa nini nasema hivyo? Ukiangalia vile ambavyo dhana zipo katika sheria zilizopendekezwa ama mswada ama rasimu iliyopendekezwa ya kubadilisha Katiba, ni kwamba sasa hatutangojea Mhasibu Mkuu wa Serikali aweze kufanya yale mahesabu na Bunge la Kitaifa kupitisha. Hapo kutakuwa na kasheshe ni pesa zipi ambazo zitakuwa asilimia 35. Kwa sababu naona muda umeyoyoma, naunga mkono. Hongera na kongole kwa wale ambao walikuwa wametusimamia, hususan viongozi wa Bunge la Seneti. Vile ambavyo tuliandamana tukaenda kule Milimani, hatukuchoka. Kuna wazee kama Mzee Ongeri ambao nilikuwa naona kwa picha nimemshika mkono. Tulikuwa pia na Mzee Amos Wako. Tukiona kama tutadhalilishwa, lakini tukasimimama na Kenya, na ninafikiri, Bunge la Seneti ni Bunge la kuwaleta Wakenya kwa pamoja. Tuwe na malumbano na sintofahamu, lakini mwishowe tutakuwa na uwiano."
}