GET /api/v0.1/hansard/entries/1028889/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1028889,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1028889/?format=api",
    "text_counter": 169,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The Temporary Speaker",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(Sen. (Dr.) Mwaura): Nafikiri kuwa Sen. (Dr.) Musuruve ametangaza msimamo wake kuhusu BBI. Yeye ni mcha Mungu kama mimi na sisi hushiriki maombi pamoja. Viti ambavyo mimi na yeye hukalia vimetupiliwa mbali katika BBI lakini viti hivyo vitarejeshwa ndio hata wengine wapate nafasi kama sisi. Walemavu wana haki zao kikatiba. Kama si hivyo, Seneti haitakuwa na mlemavu yeyote kwa sababu ni vigumu sana kwa watu walio na ulemavu kuchaguliwa, kwa sababu ya kunyanyapaliwa na kutengwa na jamii. Sasa nampa fursa Seneta mwakilishi wa vijana hapa Bungeni, Sen. Chebeni, ili pia yeye atoe maoni yake."
}