GET /api/v0.1/hansard/entries/1028944/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1028944,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1028944/?format=api",
    "text_counter": 224,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "The Temporary Speaker",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "(Sen. (Dr.) Mwaura): Asante sana, Sen. (Dr.) Milgo. Najua kuwa wewe ni mama na ukishaandaa chakula lazima ukiweke mezani. Kwa hivyo, lazima uweke hiyo Ripoti kwa meza rasmi. Ningependa kuchangia kuwa Kamati hiyo iweze kuharakisha Mswada wa watu wenye ulemavu ambao tumedhamini na Sen. Cheruiyot kwa sababu Wizara imeniambia mara mbili na hata leo ulisikia wakisema tuondoe huu Mswada na kama hilo halitafanyika kabla Bunge hii kumaliza muhula wake, itakuwa miaka kumi na tulianza huu mchakato mwaka wa 2007. Kwa hivyo, sio haki kwa watu wenye ulemavu. Sen. (Dr.) Musuruve, nafikiri kuwa tuliahirisha taarifa yako. Sijui tutafanyaje kwa sababu nilikuwa nimeshapita. Unataka kuiwakilisha rasmi?"
}