GET /api/v0.1/hansard/entries/1029013/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1029013,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1029013/?format=api",
    "text_counter": 26,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Alinukuliwa akisema kwamba vijana wa Pwani hawawezi kuajiriwa katika kazi za meli kwa sababu hawakusomea somo la Kingereza. Bw. Spika, ni jambo la kuvunja moyo kwa afisa mkuu wa Serikali katika Jamhuri yetu ya Kenya kutoa matamshi kama hayo. Katika kazi za bahari, kuna meli za Kichina, Kigiriki, Kitaliano na za kila aina ambazo zinakuja na kuondoka katika Bandari ya Mombasa. Sio lazima mtu ajue kuzungumza lugha ya Kingereza ili apate ajira katika meli hizo. Bw. Spika, Tanzania iko na chuo ambacho kinatambulika ulimwengu nzima kwa maswala ya bahari. Wakenya wengi husafiri kwenda kusomea mambo ya bahari Tanzania. Ukiangalia vizuri, lugha rasmi ya Tanzania ni Kiswahili na pia wanatumia Kiswahili kwenye Bunge. Kwa hivyo, ikiwa wanafunzi wetu wanaenda Dar es Salaam kufundishwa lugha ya Kiswahili, itakuwaje Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Usafiri kusisitiza kwamba lazima watu wasome Kingereza ndio wapate kazi kwenye meli? Bw. Spika, itakumbukwa kwamba kazi ya ubaharia imekuwa katika Mji wa Mombasa na Pwani kwa jumla kwa muda wa zaidi ya miaka 100. Vasco da Gama alipokuja mara ya kwanza kutafuta njia ya kwenda India, alishuka Mombasa na kupata wataalamu wa bahari wakamsafirisha hadi India. Kwa hivyo, swala la kuwa lazima mtu ajue lugha ya Kingereza ili kupata kazi kwenye meli halina utaalamu wowote. Kwa hivyo, Katibu wa Kudumu amekosea watu wa Pwani na vijana wa Kenya ambao wako na tamaa ya kupata ajira kwenye meli. Bw. Spika, itakumbukwa kwamba huyu Katibu Mkuu alikuwa Mkurungenzi Mkuu wa kwanza wa Shirika la Kenya Maritime Authority (KMA ). Hili ndilo shirika ambalo limepewa mamlaka ya kufunza mabaharia na kutoa vibali kwa taasisi ambazo zinafundisha mambo ya bahari. Lakini, aliondoka ofisini baada ya kuhudumu kwa muda wa zaidi ya miaka tatu bila kuweka msingi wowote wa vijana kama hawa kuweza kuajiriwa katika kazi kama hizi. Kwa hivyo, tunakemea sana kauli yake. Hafai kuendelea kutumika katika wadhifa ule kwa sababu amekaidi na kuvunja kanuni za kisheria amabazo anatakikana kutekeleza."
}