GET /api/v0.1/hansard/entries/1029019/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1029019,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1029019/?format=api",
    "text_counter": 32,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Ningependa kujiunga na wenzangu waliotangulia kuchangia Taarifa hii iliyoletwa na ndugu yangu mdogo, Sen. Anuar, Seneta mkakamavu wa Lamu. Katika sheria zetu za Kenya, hakuna mahali popote kumeandikwa ya kwamba Kizungu kitakuwa mbele ya Kiswahili. Tunavyoelewa, Kenya ina lugha mbili za kitaifa. Unaweza kuongea Kizungu au Kiswahili. Ni jambo la kusikitisha haswa ikiwa Katibu wa Kudumu anayeangalia mambo ya bahari anaweza kutamka maneno kama vile vijana wa Pwani hawajui Kizungu, na kwa hivyo hawawezi kupewa kazi kwenye meli au nyadhifa zozote zile. Hilo ni jambo la aibu. Bw. Spika, kwa mfano, mfanyikazi wako ndani ya nyumba haitaji Kingereza, ukiwa naye unaweza kutumia ishara. Kwa hivyo, ni matusi kwa mtu ambaye amepewa mamlaka na Rais wa Jamhuri ya Kenya, kutumikia Wakenya, kutukana watu wa Pwani. Jambo la aibu ni kwamba ‗ mama ‘ huyo anaishi upande wa Pwani na familia yake. Amepata utajiri wake akiwa Pwani. Bwana yake amezaliwa na kusomea Pwani. Tunaijua historia yake sana. Lakini ukarimu wetu umetuchongea mpaka anaona sisi hatufai na kuanza madharau na matusi kwa watu wa Pwani. Hili ni jambo la aibu. Ninaungana na wenzangu kusema kwamba Kamati ya Uchukuzi itakayo angalia swala hili imuite Katibu atueleze ni mahali gani ambapo pameandikiwa katika sheria za Kenya kusema kuwa kizungu ni bora kuliko Kiswahili na ndio sababu vijana wa Pwani hawawezi kupata kazi."
}