GET /api/v0.1/hansard/entries/1029342/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1029342,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1029342/?format=api",
    "text_counter": 70,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Ombi ambalo limeletwa katika Bunge na Seneta wa Kaunti ya Vihiga, Sen. Khaniri. Utamaduni ama ustaarabu ndio chanzo cha utu na ubinadamu. Ni jambo la kusikitisha kwamba kwa sasa tumeweza kuweka ustaarabu na utamaduni wetu nyuma kiasi ambacho vizazi vijavyo huenda vikapotea na vikawa havina mwelekeo. Kwa mfano, Mombasa ilikuwa ni kitovu cha ustaarabu wa Waswahili. Kule ndiko lugha ya Kiswahili ilianza kuzungumzwa na ikasambaa sehemu za bara. Ni masikitiko makubwa kwamba hata zile taasisi za zamani ambazo zilisaidia kukuza na kuendeleza utamaduni huu hazipo tena. Bi Naibu Spika, kaunti zote katika Kenya hazitilii mkazo swala la utamaduni. Mwaka uliopita nilibahatika kusafiri na Bw. Spika kwenda Kaunti ya Tana River kusheherekea siku ya utamaduni wa Wapokomo, Waoroma na jamii zingine ambazo zinaishi huko. Tukio kama hili ni nadra katika kaunti zingine hapana. Ombi hili la Sen. Khaniri limekuja katika wakati mwafaka. Tunaona kwamba maadili yanaendelea kubomonyoka kutokana na kuiga kwa wingi tamaduni za watu wengine. Lugha ya Kiswahili ina tamaduni zake ambazo hujumuisha nyimbo, michezo, mashairi na ngojera na kadhalika. Hayo yote husaidia kukuza na kuendeleza utamaduni wa Waswahili. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}