GET /api/v0.1/hansard/entries/1029343/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1029343,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1029343/?format=api",
"text_counter": 71,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bi. Naibu Spika, jengo la Fort Jesus katika Mji wa Mombasa ni la kale sana. Wanahistoria husema lilijengwa karne ya 15. Sasa hivi ni mahame na magofu. Hakuna watalii wa kutoka nje wanaozuru jumba hilo kwa sababu halijawahi kufanyiwa ukarabati wowote. Juzi ufuo wa bahari wa Mama Ngina ulifanyiwa ukarabati. Wakati walipokuwa wakifanya ukarabati huo, kulipatikana makaazi au mijengo ambayo ilijengwa karne ya 12. Ni lazima tutilie mkazo swala la kulinda na kuhifadhi tamaduni kwa sababu ya vizazi vijavyo. Bi. Naibu Spika, kila kabila au jamii yoyote ina tamaduni zake. Lazima tuheshimu tamaduni za jamii zingine kwa sababu ndio mwanzo wa kuweza kuheshimu tamaduni zako. Ukiwa wewe huwezi kuheshimu tamaduni za watu wengine, basi zile zako pia huwezi kuziheshimu. Ni lazima tuheshimu na tuhifadhi tamaduni zetu ili vizazi vijavyo viwe na mwelekio mzuri wa Kiafrika. Asante kwa kunipa fursa hii."
}