GET /api/v0.1/hansard/entries/1029348/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1029348,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1029348/?format=api",
"text_counter": 76,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Jambo la pili ni kuwasihi waheshimiwa Wabunge kukuza na kuhifadhi tamaduni zetu. Ikiwa nchi mzima inatuangalia sisi kama watu ambao tumeweza kufahamu mambo ya utamaduni, ni muhimu hili Bunge lichukue nafasi hiyo liwe kipau mbele kueleza mambo haya. Bi Naibu Spika, historia ya Bunge hili haijanukuliwa vizuri. Kwa mfano, hapa tuna kaburi la Mzee Jomo Kenyatta; mwanzilishi wa Taifa la Kenya. Katika mataifa mengine, makaburi ya waanzilishi wa mataifa yao, watalii huyazuru na kuelewa historia ya taifa hilo. Huko ndiko wao hufahamishwa vile kiongozi aliyekuwa wa kwanza kuanzisha nchi hii alikuwa anaishi namna gani, aliweza kuongoza nchi namna gani na historia na kadhalika. Bi Naibu Spika, lakini kaburi la Mzee liko kule pembeni na hata waheshimiwa Wabunge hapa hawawezi kulifikia. Kaburi hili ni kama la familia. Kama ni kaburi la familia lisingewekwa katika mazingira ya Bunge. Ingekuwa vizuri kama sisi katika utamaduni wetu tungeweza kuwaelemisha watalii na watu wengi umuhimu wa kaburi hili na historia ya taifa hili. Kaburi hili lingekuwa mfano na kielelezo kama utamaduni wa kwanza wa taifa hili. Bi Naibu Spika, nilipozuru hapa Bunge mara yangu ya kwanza, niliona viti vya zamani vya Spika. Tuliweza kuona vinyago vya spika na vitu vingine vya utamaduni wa Bunge. Wakati huu tunarekebisha mambo na kuharibu historia ya Bunge hili. Hakuna kilelezo chochote kuhusu kiti ambacho Spika wa kwanza alikitumia. Kiti ambacho kililetwa na Wakoloni, hakipo. Hakuna tamaduni zozote ndani ya Bunge hili letu la Kenya. Nafikiria ingekuwa muhimu pia kuangalia tamaduni kama hizo. Bi Naibu Spika, sisi kama wamiijikenda kutoka maeneo ya pwani, tuna nguo zetu zinazoitwa mahando ambazo tunafaa kijivunia, lakini nguo hizo zinaonekana kama mambo ya zamani na kwamba hayawezi kutumika hivi sasa. Wazee wetu wa zamani walikuwa wanaenda mahali kama Kaya Fungo kuomba Mungu, lakini hali sio hivyo sasa. Maeneo kama haya sasa yametengwa. Hakuna hata barabara ya kuenda Kaya Fungo. Serikali ingalikuwa inazingatia mambo ya utamaduni, ingalitilia mkazo kuona kwamba barabara za kuenda mahali kama Kaya Fungo zimetengenezwa. Vasco da Gama Pillar iliyoko Malindi ilijengwa katika Karne ya 15 katika mwaka wa 1498, lakini idadi ya Wakenya wanaotembelea sehemu ile ni kidogo sana. Hiyo ni kwa sababu Serikali haijazingatia mikakati ya kuhakikisha kwamba tumeipa utamaduni wetu kipaumbele. Nasisitiza kwamba Serikali ya Kenya inafaa kuwajibika katika kuhifadhi utamaduni wetu. Asante sana."
}