GET /api/v0.1/hansard/entries/1029409/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1029409,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1029409/?format=api",
    "text_counter": 137,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kuambatana na Kifungu cha 48 (1) cha Kanuni za Kudumu za Seneti, kuomba Taarifa kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Leba na Ustawi wa Jamii kuhusu kuteuliwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Bahari, KenyaMaritime Authority. Kwenye Taarifa hiyo, Kamati inafaa: (1) Kufafanua sifa zilizohitajika kwa mwombaji wa wadhifa huo wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Bahari. (2) Kuelezea idadi ya wakenya waliowasilisha maombi yao kwa wadhifa huo. (3) Kutoa ripoti kuhusu waliobobea kwenye mahojiano na waliowasilisha maombi ya kutwaa wadhifa huo. (4) Kuelezea sababu ya Waziri wa Barabara na Uchukuzi kumteua Bw. Njue Robert Mutegi ambaye alikuwa wa nne kwenye mahojiano hayo, hivyo basi kutostahili kupewa wadhifa huo."
}