GET /api/v0.1/hansard/entries/1029419/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1029419,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1029419/?format=api",
"text_counter": 147,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": ", anayeitwa James Njiru. Vile vile, kuna Katibu wa Kudumu katika State Department ambayo inahusika na mambo ya uvuvi na Blue Economy ambayo ni mambo ya samaki na bahari ambayo yanahusikana na ufuo wa Pwani. Nafasi hiyo, ikachaguliwa mtu anaitwa Michemi Ntiba. Bi. Naibu Spika, wa mwisho ni Katibu wa Kudumu ambaye tunaweza kusema anahusika na mambo ya Maritime Shipping ambaye anaitwa Nancy Garikithu. Bi. Naibu Spika, watu hawa wote niliowataja hapo watano, wanatoka katika eneo moja katika nchi yetu ya Kenya. Kazi zote tano zinahusikana na watu wa Pwani. Ni jambo la kukasirisha sana. Hivi leo, tumeona nafasi kama tano zinatoka na zote tano hakuna hata mtu mmoja wa Pwani ambaye amepewa nafasi hii. Ni aibu kwa yule aliyechagua na kwa wale wanaoketi katika lile baraza kwa kusema kwamba ‘weka huyu mtu hapa awe mkubwa wa Bandari Maritime Academy ; weka akuwe mkubwa katika Maritime Fisheries and Research Institute ; weka hapa akuwe mkubwa wa Blue Economy .’ Bi. Naibu Spika, sisi kama watu wa Pwani tuko na haki katika hii nchi. Hatuwezi kukubali kuachwa nyuma hata kidogo. Kama nafasi zimetokea kuhusu mambo ya Pwani, ni lazima watu wa Pwani wapewe kipao mbele kwanza. Ni aibu hivi leo mimi kusimama hapa mbele ya hii Seneti na kuona ya kwamba katika hii orodha watu wote watano waliochaguliwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye anatoka eneo la Pwani na hizi kazi zote ziko eneo la Pwani. Wale wanaochagua hawa watu wakiongozwa na Waziri wa Usafiri, Bw. Macharia, tunasema ya kwamba kitu kama hiki kisiletwe mbele yetu hata kidogo. Asante Bi. Naibu Spika."
}