GET /api/v0.1/hansard/entries/1029423/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1029423,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1029423/?format=api",
"text_counter": 151,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Malalah",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13195,
"legal_name": "Cleophas Wakhungu Malalah",
"slug": "cleophas-wakhungu-malalah-2"
},
"content": "Asante Bi. Naibu Spika. Nitajikaza kisabuni kuhakikisha kwamba nimeongea kwa lugha ya Kiswahili. Ningependa kumjulisha Sen. Madzayo na Seneti hii kwamba pia zile huduma za bandari tayari zimeshatolewa na kupelekwa Naivasha. Pia, kuna shurutisho kwamba mizigo zote zisafirishwe kwenye reli. Ningependa kumwambia akuwe na habari iyo ili wakati anachangia atuambie yale machungu ambayo watu wa Pwani wako nayo. Sisi kama viongozi wa Seneti, ni jukumu letu kuhakikisha kuwa kuna usawa hapa Kenya. Kenya iko na makabila 43 na ni lazima usawa na haki ufanyike hapa Kenya. Sisi tungependa kuunga mkono ndugu zetu wa Mkoa wa Pwani. Si hao pekee wanaumia. Pia sisi kule eneo la Western tunaumia kwa sababu tuko na mashirika kama Lake Victoria South Water Works Development Agency. Katika bodi nzima ni kabila moja tu ambalo limeketi. Watu wa uliokuwa Mkoa wa Magharibi hawajawakilishwa katika bodi hiyo."
}