GET /api/v0.1/hansard/entries/1029495/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1029495,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1029495/?format=api",
"text_counter": 223,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia taarifa ya Sen. Malalah kuhusiana na ugonjwa wa COVID-19. Ni masikitiko makubwa kwamba nchi yetu imeendelea kuona mkurupuko wa visa zaidi vya COVID-19 vinavyosababisha vifo. Nikizungumzia Kaunti ya Mombasa ninapotoka, ni jambo la kusikitisha kuwa karibu kila siku kwa muda wa siku 10 nimekuwa nikishuhudia visa vya watu wanaofariki ambao wengine ni watu walio karibu na mimi. Nikizungumzia wiki iliyopita, siku ya Jumamosi, diwani wa zamani wa eneo la Majengo anayeitwa Said Mathias alifariki. Bunge la Kaunti ya Mombasa limefungwa sasa kwa sababu kulipatikana visa nane vya maambukizi ya COVID-19. Watu wengine wengi wanazidi kuathirika na kuaga dunia kwa sababu ya COVID-19. Huduma za afya pia zimeendelea kuzorota kwa sababu hospitali zote ikiwemo hospitali kuu ya Mkoa wa Pwani zimejaa wagonjwa wanaohusiana na Korona. Vifaa vya matibabu katika Kaunti ya Mombasa vimeathirika pakubwa kwa sababu madaktari pia wameathirika na ugonjwa. Wauguzi wanaohudumia wagonjwa wameathirika na ugonjwa huu. Kwa hivyo, hali imekuwa tete sana katika Kaunti ya Mombasa."
}