GET /api/v0.1/hansard/entries/1029496/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1029496,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1029496/?format=api",
    "text_counter": 224,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bwana Spika wa Muda, hapo nyuma kidogo tuliweza kuteteleka na tukawacha kufuata yale maagiza ambayo yametolewa. Kwa mfano, tuliruhusu watu kukutana kiholela, kutembea mijini bila barakoa na kutotumia kitakasa. Hivi Sasa, hali ambayo inatokea katika maeneo ya burudani na sehemu zingine ni kuwa watu wanaendelea kusongamana kwa wingi bila kuchukua tahadhari zozote. Ni masikitiko kwamba hali imekuwa hivi na hatuwezi kuendelea kulalamika kuhusu hali hii bila ya kuchukua hatua mwafaka. Bw. Spika wa Muda, nimefurahi kwamba leo Rais ameweza kurejesha amri ya kutotoka nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri. Lakini hiyo haitoshi. Hii kwa sababu bila ya askari kuhakukisha kwamba maagizo ya amri ya kutotoka nje yanafuatiliwa itakuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Utapata kuona maeneo mengi ya burudani yanaendelea kutoa huduma kwa wananchi baaada ya masaa ya amri ya kutotoka nje na hakuna jambo lolote ambalo litafanyika. Pia, tumeona kwamba kumekuwa na ulegevu katika vitengo vya huduma za afya. Kwa mfano, katika idara za afya ya umma hazijachukua hatua mwafaka za kuhakikisha kwamba wanaendelea kuwaelemisha wananchi maswala ya huduma ambazo zinatakikana kufanyika ili kuhakikisha kwamba mtu hawezi kupata Korona. Tungeweza kurudi hapo katika idara za afya za umma ili wahakikishe kwamba wananchi wanajulishwa. Zile sehemu ambazo watu wameathirika na ugonjwa huu waweze kutiliwa maanani zaidi ili kuhakikisha kwamba mkurupuko huu hauwezi kuendelea. Bw. Spika wa Muda, kuna dawa ambazo zinaweza kutumika. Si tiba lakini zinawezakutumika kwa wale ambao wameweza kupata maambukizi lakini hawajaonyesha ishara za ugonjwa. Hii pia ingeweza kusisitizwa ili kuhakikisha kwamba wale ambao wameamua kujihudumia nyumbani--- The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}