GET /api/v0.1/hansard/entries/1029501/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1029501,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1029501/?format=api",
    "text_counter": 229,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bwana Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Ikiwa tuko kipaumbele kuongea habari ya mambo ya korona, ni lazima Bunge hili lenyewe liwezekutimiza hizo sheria za Korona. Nikasisitiza habari ya utamaduni tukasema kwamba Bunge lazima lichukue mkondo wa mbele kwa mambo ya utamaduni. Tukija upande wa Wabunge na Korona, unaweza kuona barakoa hii ambao nimeishika kwa mkono wangu wa kushoto ni ile ambao tulinunua nje kwa shilingi mia moja. Lakini kuna uzembe unaendelea hapa ndani ya Bunge. Barakoa hizi ni bandia. Hata barakoa zinazovaliwa na makarani wetu ni bandia. Ni vitambara ambavyo vimetengenezwa kule River Road na viweze kuzuia usambasaji wa Korona. Bei yake ni chini mno na inaashiria ubandia wake. Sisi kama Bunge hatuchukulii ugonjwa huu kwa umakinifu sana. Barakoa hizi haziwezi kufananishwa na barakoa ya N95. Bw. Spika wa Muda, haya ni madharau ya hali ya juu. Sisi ni Wabunge na waheshimiwa wa kitaifa. Barakoa hizi zinaweza kusababisha kuenea kwa ugonjwa huu na waheshimiwa wengi hapa Bungeni kufa. Jambo hili lichukuliwa kwa umakinifu kwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}