GET /api/v0.1/hansard/entries/1029859/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1029859,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1029859/?format=api",
    "text_counter": 259,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. (Bi.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na dadangu Mhe. Wamaua. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa hakika stakabadhi hii tunaita birth certificate, ni muhimu sana na ni cheti cha kwanza mtoto hupata akizaliwa. Stakabadhi hii ndiyo itaonyesha umri wa mtoto huyu ambaye amezaliwa katika Taifa letu la Kenya. Tumeona changamoto nyingi sana ambazo Wakenya wengi wamepata kupata stakabadhi kama hizi, haswa tukiangalia wenzetu kutoka kule sehemu za North Eastern. Wamekuwa na changamoto nyingi sana. Hata kule kwetu Mombasa imekuwa ni changamoto kupata stakabadhi kama hii. Stakabadhi kama hii hivi sasa imepata umuhimu kiasi kwamba wanafunzi hawawezi kufanya mitihani katika shule zao kama hawana stakabadhi hiyo."
}