GET /api/v0.1/hansard/entries/1029865/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1029865,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1029865/?format=api",
"text_counter": 265,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Mhe. (Bi.) Mishi Mboko",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Ukifika katika ofisi zile, kwanza utaulizwa utoe stakabadhi hii ya birth certificate. Nataka niseme imekuwa ni changamoto kwa sababu si wazazi wote ambao wanajifungua ama wanazalia katika hospitali zetu ambapo watapata kile cheti kiitwacho birth notification. Wazazi wengi ama akina mama wengi wanaweza kujifungua kupitia wakunga kule manyumbani ama kule nyanjani. Hivyo, inakuwa changamoto kuweka zile takwimu ama mawasiliano katika zile asasi zetu muhimu ili zinukuliwe na kupata takwimu za mtoto yule ili aweze kupata stakabadhi kama hii. Nasema kwamba huu ni wakati mwafaka ambapo teknolojia imebobea. Wakati teknolojia imebobea, lazima pia twende na muondoko huo huo wa kwamba hata sisi pia tumebobea katika teknolojia. Hivyo basi kuwa na ile centre ambayo tunasema ni database centre, mahali ambapo mawasiliano yote ama zile takwimu zote zinazohusu stakabadhi nyeti na muhimu kama hizi zitakuwa pahali pamoja na kugatuliwa kule chini mashinani. Juzi tulifungua ile tunaita Huduma Centre, mahali ambapo tunaweza kupata huduma tofauti tofauti ikiwemo stakabadhi hii tunayoizungumzia sasa. Lakini tunaona kwamba hizi Huduma Centre zimewekwa katika sehemu za mijini ama ile miji mikubwa. Pia inakuwa changamoto kwa wazazi ama Wakenya wengi kuweza kufika pale ili kupata stakabadhi kama hizi. Iwapo tutaweza kupata hizi database ambazo zitakuwa kule nyanjani katika yale maeneo ya uwakilizi katika bunge letu ama kwa Kingereza our sub-counties, itakuwa ni sehemu ambayo hakuna Mkenya atakuwa na matatizo kupata stakabadhi kama hizi. Pia tumekuwa na changamoto kwa sababu utapata watu ambao sio wakenya wanataka kupata stakabadhi za Kenya kupitia njia za ufisadi. Tukiwa na hifadhi ya data kama hii, mambo hayo yatachujwa ili kuhakikisha kwamba watu ambao wanapata stakabadhi hii ni walengwa, wahusika na watu ambao wamezaliwa katika taifa letu la Kenya. Tukitimiza Hoja kama hiiā¦"
}