GET /api/v0.1/hansard/entries/1030103/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1030103,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1030103/?format=api",
    "text_counter": 191,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Igembe South, Independent",
    "speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
    "speaker": {
        "id": 1574,
        "legal_name": "Cyprian Kubai Iringo",
        "slug": "cyprian-kubai-iringo"
    },
    "content": " Asante sana, Bwana Spika. Nasimama kuunga mkono ripoti hii, lakini nitaenda kinyume na wale ambao wanasema kwamba vijana hawana ujuzi wa kazi hii ya ubalozi. Hii ni kwa sababu wakati ambapo taifa hili lilifanya uchaguzi mwaka wa 2013, Rais na Naibu wake hawakuwa wamefikisha umri wa miaka 60, lakini Wakenya waliona kwamba walikuwa na ujuzi wa kuongoza taifa hili na ndiposa waliwapa nafasi hiyo. Kwa hivyo, ile dhana ambayo kila mmoja akisimama anasema kwamba vijana hawana ujuzi, sio ukweli. Wakati huu pia tuko na gavana ambaye ana umri wa miaka 30. Watu wa hiyo kaunti walimchagua kwa sababu walijua kwamba ana ujuzi na ataweza kupeleka kaunti hiyo mbele kwa kufanya kazi kwa manufaa ya wakaazi wa kaunti hiyo. Kwa hivyo, wakati ambapo mtu amefikisha umri wa kustaafu, ni vizuri apewe nafasi hiyo apumzike halafu wale vijana barubaru ambao wako na uwezo wa kufanya kazi hiyo wapewe hiyo kazi wafanye. Hii ni kwa sababu, kila wakati ambapo uteuzi unafanywa, wale watu ambao huwa wanapewa hizi nyadhifa ni wale wamefikisha umri wa kustaafu. Jambo hili linatendeka ilhali tunajua kuwa watu wengi ambao wako na ujuzi wa kutosha wako nyumbani kwa sababu ya ukosefu wa ajira. Kwa hivyo, wanafaa wapewe nafasi ili watekeleze ama kuonyesha ujuzi wao. Wakati ambapo tunawatuma hawa mabalozi katika hizo nchi za kigeni, ni vizuri wawe katika mstari wa mbele wa kuwakilisha Kenya katika masoko ya nchi hizo ili tuweze kuuza bidhaa zetu za kilimo. Tumeona nchi nyingi ambazo zinasusia kufanya biashara na nchi hii ilhali tuko na mabalozi ambao wanawakilisha taifa hili katika mataifa hayo. Pia, kuna nchi nyingi ambazo vijana wetu wanaenda kutafuta ajira na wanafungwa huko ilhali tuko na mabalozi kule ambao wanafaa kuwakilisha taifa hili na kutetea hao vijana wakati ambapo kuna shida kama hiyo. Kwa hivyo, mtu akipewa kazi hii, ni jukumu lake kuifanya kwa niaba ya watu waliomtuma kufanya kazi hiyo. Wale watu ambao tunatuma kwa hizo nchi ni wazee. Ni matarajio yangu kuwa, katika masomo, wakati ambapo..."
}