GET /api/v0.1/hansard/entries/1030116/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1030116,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1030116/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Changamwe, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Omar Mwinyi",
    "speaker": {
        "id": 1345,
        "legal_name": "Omar Mwinyi Shimbwa",
        "slug": "omar-mwinyi-shimbwa"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii. Kwanza, nasimama kupinga uteuzi huu kwa sababu zifuatazo: Kenya si taifa changa kwa sababu lina miaka 57. Ni mtazamo wa sisi sote ambao tuko katika nchi hii ya kuwa ni lazima tujue kuwa sisi ni Wakenya na usawa tunaozungumza kwenye mikutano yetu ya BBI uko dhahiri. Ukiangalia haya majina, ikiwa tuna makabila 43 katika nchi yetu ya Kenya na uone majina ya sehemu moja ni mengi ilhali sehemu nyingine hazipo kabisa, je, ni kwa nini tuunge mkono uteuzi huu? Sioni muislamu hata mmoja kwenye uteuzi huu ilhali tuna karibu asilimia 40 ya waislamu. Tunazungumzia kuhusu watu kushirikiana na kutangamana lakini leo mabalozi 14 wanachaguliwa na hakuna hata muislamu mmoja. Ninashangaa sana kwa nini wenzangu wanaunga uteuzi huu mkono. Tunaunga nini mkono? Tuna Wahindi, Waarabu na makabila tofauti, kwa nini hawako hapa? Sisi sote ni Wakenya. Ni wakati tunataka kuona kuwa katika uteuzi wa aina yeyote, Wahindi, Waarabu na makabila mengine yanatambuliwa ili watu wote wajisikie na kujivunia kuwa Wakenya. Tunavyozungumza, tunajiona sisi ni wageni, hatuna haki na hakuna usawa katika hii nchi. Nitakukumbusha tu siku za Hayati Moi ambapo baada ya uchaguzi, tulikuwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ardhi kutoka Pwani, lakini hayo hayafanyiki hivi leo. Tunapewa tu nafasi moja ya Wizara ya Utalii na ni kwa mtu ambaye hana uhusiano na watu; ni yeye peke yake na Baraza la Mawaziri. Nawaomba Wajumbe wenzangu kuipinga Ripoti hii. Mhe. Spika, Mombasa ni kitovu cha Taifa letu na hakuna jambo litafanyika bila kuihusisha na kuunga mkono lakini leo hii tunatumiwa tu. Hatufaidi hata kwenye uteuzi kwenye mashirika yaliyo Mombasa. Hivi majuzi, Katibu Mkuu ambaye amelelewa Mombasa alikuja na kututusi kuwa watu wa Pwani hawapati kazi kwa sababu hawajui Kiingereza. Ni nani alikwambia Kiingereza tu ndio lugha ya kufanyia kazi? Wachina hii leo wanajenga mabarara ilhali hawajui Kiingereza. Hivi majuzi, uteuzi wa Mkurugenzi wa Kenya Maritime Authority ulifanyika, na kijana kutoka Mombasa ambaye ni wakili akaachwa…"
}