GET /api/v0.1/hansard/entries/1030499/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1030499,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1030499/?format=api",
    "text_counter": 193,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Sifa kubwa ya kiongozi ni kwamba lazima awe mtu wa kuheshimu sheria na binadamu wengine, lakini kitendo Prof. Magoha alifanya kinakiuka maadili hayo. Sote tuna mapungufu katika utendakazi wetu, na itakuwa si sawa kwa kiongozi yeyote kumuita mwenzake mjinga ama mpumbavu akiwa hadharani penye kila mtu anaweza kuona. Hayati Julius Nyerere alisema kwamba mtu mpumbavu amezaliwa mpumbavu. Yaani, kwa Kiingereza, he is a fool. Mjinga ni yule ambaye hana ufahamu wa jambo fulani. Kwa hivyo, akifahamishwa, ule ujinga huwa unaondoka. Bi. Naibu Spika, kama kulikuwa na jambo ambalo Waziri aliona kuwa kuna na upungufu kwa yule afisa wa elimu, angemwita faraghani na kuweleza, “Jambo hili linafaa kufanywa kwa njia ifuatayo.” Lakini kumwita mjinga ama mpumbavu mbele ya hadhara ni jambo ambalo ni kunyime na maadili. Kwa hivyo, ninamkemea Waziri Magoha kwa jambo kama hili. Jambo ambalo linavunja moyo ni kwamba hiyo habari imesambazwa katika vyombo vya habari na imefikia familia na watoto wa afisa huyo wa elimu. Hao pia sasa wanamdharau mzee wao ambaye ni kiongozi wa familia yao. Ninakemea jambo hilo. Naomba dakika moja nionge kuhusu arifa iliyozungumziwa na Seneta Nyamunga. Jimbo la pwani limeathirika sana na uuaji wa wananchi. Wengi wao wameuawa na taasisi za serikali na hatujui chanzo ya hizo vifo. Kamati ya sheria na haki za kibinadamu ya Seneti ilikuwa imevamia jambo hilo na ilifanya kikao kule pwani na ni jambo lakusikitisha kwamba watu bado wanaendelea kupotea hadi sasa. Lazima jambo hili lifuatiliwe kwa haraka ili ripoti ya Kamati ya Sheria na Haki za Kibinadamu ya Seneti iletwe hadharani na wahusika washtakiwe na kupelekwa mahakamani kwa wakati unaofaa. Ni jambo la aibu kwamba tuna Katiba nzuri ambayo tulipitisha mwaka wa 2010 lakini watu wamepotea wengi tukiwa na hii Katiba kuliko wakati tulikuwa na katiba ya kitambo. Asante, kwa kunipa hii nafasi."
}