GET /api/v0.1/hansard/entries/1030556/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1030556,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1030556/?format=api",
"text_counter": 250,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Ningependa kuchangia Hoja ya Nidhamu ya Sen. Wambua kwamba, kuna Taarifa za Maseneta za kibinafsi na kuna zingine za Kamati ambazo tunafaa kuzipea kipaumbele. Mwenyekiti wa Kamati hawezi kukaa mpaka saa hii ambapo tunajadili Taarifa za kibinafsi. Mwenyekiti wa Kamati anaweza kuwa na Taarifa ya Kamati ambayo ni muhimu zaidi kuliko Taarifa ya kibinafsi. Wakati tunapanga ule wakati, tungezingatia jambo hilo kwa sababu zile Taarifa ambazo zinasomwa hapa, kwa mfano, nimekaa hapa kutoka saa nane unusu na niko na Ripoti ya Kamati na vilevile niko na Hoja ambayo nimepeana na mpaka hivi sasa, 5.30 p.m., sijapata fursa ya kuzungumzia Hoja hii. Tukiendelea hivi, itakuwa inatuvunja moyo wengine wetu ambao ni Wenyekiti wa Kamati, kwa sababu tunafungwa hapa Seneti bila kutoa mchango wowote wa kisawa sawa. Nikirudia Taarifa ya Sen. Were, ningependa kuunga mkono Taarifa hii. Imekuja wakati mwafaka kwa sababu tumeona kuwa Safaricom PLC inaendelea kutumia ueledi na ukubwa wake katika soko la mawasiliano kuwagandamiza wale ambao wanataka kufanya biashara hiyo na kutupa huduma duni, sisi watumizi wa huduma hiyo. Bw. Spika wa Muda, ukiangalia baadhi ya bidhaa ambazo Safaricom wanauza, kwa mfano, wanauza airtime au muda wa maongezi na data . Inapofika kiwango fulani, ile nafasi ama kasi ambayo inatakikana kutumika katika ile data umepewa inapungua. Hii ni kwa kusudi, kwa sababu wanajaribu kupunja wateja wao kuhusiana na bidhaa ambazo wanawapatia."
}