GET /api/v0.1/hansard/entries/1030944/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1030944,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1030944/?format=api",
"text_counter": 315,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kwa mfano, Ofisi ya Rais itakuwa na fursa ya kuchagua Waziri Mkuu na kumfuta wakati wowote wanapotaka. Hizo ni nguvu zaidi ambazo zitaongezwa kwa Ofisi hiyo kuliko vile ilivyo sasa kwa sababu hakuna nafasi ya Waziri Mkuu kwenye Katiba. Sisi katika Seneti lazima tuangalie mapungufu tuliyonayo na jinsi tutaongeza nguvu zetu ili Seneti itakayofuata iwe na nguvu na mamlaka zaidi ya kutekeleza kazi yake ya kutetea ugazuti katika nchi yetu ya Kenya. Wanapendekeza kuongeza Maseneta wengine 47 wa jinsia ya pili. Sio kwamba tunaongezewa nguvu; ni kupewa idadi ya watu ambayo haitasaidia popote katika kutetea ugatuzi katika nchi yetu. Kwa kumalizia, ofisi za wawakilishi wa wanawake zinapoteza zaidi ya Kshs2 billion kwa mwaka. Ukifanya hesabu, Kshs6 million kwa maeneo mbuge 290 ni Kshs1.7 billion kila mwaka. Tunafaa kujiuliza pesa iliyotakikana kwenda kwa akina mama inakwenda wapi. Badala ya kuteta katika Seneti eti tunataka Maseneta 47, ata wawe 100 tuko tayari. Tunataka kujua, hii Shilingi 1.7 bilioni ambayo Serikali itatoa katika ofisi za"
}