GET /api/v0.1/hansard/entries/1030947/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1030947,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1030947/?format=api",
"text_counter": 318,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bi. Naibu Spika, kwa kumalizia, wabunge waliochaguliwa hapo mbeleni kwa viti tofauti katika Bunge wamefanya kazi kubwa kupeleka mbele miswada inayo husu akina mama kuliko wale tunao sasa. Huo ndio mjadala tunataka kuangalia. Ni njia gani tutatumia kusukuma mbele mjadala wa akina mama, ili haki zao na za watoto wetu wa kike zilindwe? Vili vile, pia bibi zetu wapate haki sawa katika Katiba yetu. Mjadala si kwa nini awe mume ama mke, mjadala ni vipi tutaweza kuongeza nguvu za Seneti ili liheshimike inavyo takikana."
}