GET /api/v0.1/hansard/entries/1031017/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1031017,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1031017/?format=api",
    "text_counter": 388,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Nimesimama kupinga Mswada huu wa kubadilisha vikao vya Bunge kutoka Jumanne, Jumatano na Alhamisi mpaka Jumanne ambayo ni siku moja kwa wiki. Nimekuwa hapa kutoka jana na Ripoti muhimu ya kamati yangu. Jana nilikaa hapa kuanzia saa nane unusu mpaka saa kumi na mbili unusu tulipoahirisha kikao. Sikuweza kupewa fursa ya kuweza kuendeleza hiyo Ripoti. Leo vile vile, nimekuwa hapa kutoka saa nane na nusu mpaka saa hii, saa kumi na mbili, na sijaweza kupata fursa ya kuendeleza Ripoti yangu. Bi Spika wa Muda, hii inamaanisha kwamba wakati ambao tuko nao katika Bunge ni mchache na haitatuwezesha sisi kukamilisha ratiba ya kazi ambayo inatakikana kufanyika kwa ile siku ambayo tunakaa. Kwa hivyo, iwapo tutapunguza vikao na iwe ni kikao kimoja kwa wiki, ina maana kwamba kutakuwa na msongamano wa kazi inayofanyika hapa katika Bunge la Seneti. Hiyo itamaanisha kwamba kazi nyingi itachelewa. Maseneta ambao wanashughuli zao katika Bunge hili wataweza kuvunjika moyo na hawataweza kuhudhuria vikao. Bi Spika wa Muda, ijapokuwa tunatahadhari kwamba ugonjwa wa COVID-19 upo, na umeweza kuathiri baadhi ya watu wetu, lakini vile vile, ni kwamba, hata kikao cha mara moja kwa wiki kinaweza kusababisha maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19. Kwa hivyo, itakuwa siyo salama kwa Wabunge kuhudhuria hata kama ni kikao kimoja. Nimesimama kupinga Hoja hii ya kuahirisha vikao na kuwa na kikao kimoja kwa wiki kwa sababu hautasaidia pakubwa kupunguza kazi ambayo tuko nayo mbele ya Bunge kabla ya vikao kuahirishwa 2.12. 2020. Bi Spika wa Muda, naongezea tu kwamba, ni muhimu kwamba, kwa vile tunafikia mwisho wa mwaka, tuweze kuzingatia zile kazi ambazo zilikuwa zimeratibiwa kufanyika, zifanyike ili tukiondoka kuenda mapumziko ya Krismasi na mwaka mpya, tuwe tumemaliza kazi zetu ambazo zimeweza kupangwa. Kwa kumalizia, nasema kwamba, wale ambao wameathirika na ugonjwa huu, tunawatakia afueni ya haraka. Lakini pia ni kuwa, tukifunga Bunge ama tukiwa na vikao vichache, hatutaweza kukamilisha kazi yetu ya kuweza kuchunguza na kuangalia Serikali kwa wakati huu mgumu wa COVID-19, hususan huu wakati ambapo sasa limekuja shambulio la pili la haya maradhi."
}