GET /api/v0.1/hansard/entries/1031019/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1031019,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1031019/?format=api",
"text_counter": 390,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante Bi Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Nimesimama kupinga Hoja iliyotolewa ili kuahirisha Bunge na kuweka siku moja kwa wiki. Vile msemaji aliyenitangulia, Seneta wa Kaunti ya Mombasa alivyosema, kwa hakika, hata siku moja tukikaa katika kikao hapa, kama maambukizi yatakuwa yanaendelea, basi hata hiyo siku moja, maambukizi yanaweza kuendelea. Tuko mwezi wa kumi na moja na tuko na kazi nyingi ambazo bado zinasalia katika Bunge. Tukipunguza kwa siku moja, hiyo inamaanisha kwamba, kazi nyingi ambayo ingeweza kufanyika mwaka huu itavuka kuenda mwaka ujao. Bi Spika wa Muda, mambo muhimu kama Building Bridges Initiative (BBI) saa hii inaendelea kuzungumzwa. Kama Bunge hili litakuwa na siku chache, Wakenya kule nje watavunjika moyo sana, kwa sababu watu wako na imani sana na Bunge la Seneti kutokana na vile ambavyo tulifanya mambo ya ajabu na kuweza kuleta moyo wa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}