GET /api/v0.1/hansard/entries/1031020/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1031020,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1031020/?format=api",
"text_counter": 391,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Wakenya wote pamoja. Imani yao ni Bunge hili la Seneti liweze kufanya kazi yake kwa siku tatu. Nilikuwa nikiomba leo yote ili niweze kuongea, lakini sikupata fursa hiyo. Hiyo inamaanisha kwamba, kuna msongamano wa maombi mengi katika Bunge hili. Ndio sababu sisi tunasalia kuendelea kuomba na hatupati nafasi hiyo. Bi. Spika wa Muda, kwa hivyo, tusijinyime hiyo haki ya kuzungumza mambo ya watu wetu katika Bunge hili. Mambo ya maambukizi ya COVID-19 kusema ukweli yako duniani kote. Mimi ninaona huu ugonjwa hautaondoka hapa nchini Kenya. Kama wakati ule tulifunga shule, vyuo vikuu, misikiti na makanisa ilhali huu ugonjwa bado unasambaa. Leo hata tukifunga Bunge, makanisa na misikiti, huu ugonjwa bado utatufuata. Kwa hivyo, tusitoroke kwa ule ukweli na tusiwe waoga wa kuenda kwa siku moja ama kufunga Bunge hili. Hilo halitakuwa suluhisho. Bi Spika wa Muda, tusimame kidete na tuweze kuleta mikakati ambayo ni ya kupigana na ugonjwa huu ili tuweze kuumaliza. Tukitoroka huu ugonjwa, basi itakuwa sio suluhisho na mambo yote yataendelea kudorora. Nimesimama kupinga."
}