GET /api/v0.1/hansard/entries/1031358/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1031358,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1031358/?format=api",
"text_counter": 313,
"type": "speech",
"speaker_name": "Igembe South, Independent",
"speaker_title": "Hon. John Paul Mwirigi",
"speaker": {
"id": 1574,
"legal_name": "Cyprian Kubai Iringo",
"slug": "cyprian-kubai-iringo"
},
"content": " Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Nimesimama kuunga mkono Ripoti hii kwa sababu ya madhara mengi ambayo yameangaziwa hapa. Madhara ni mengi wakati ambapo msichana ama mtoto wa kike anapitia hali hii ya ukeketaji.. Katika hali hii, tumesikia kwamba, wakati mtu anapitia haya, huvuja damu nyingi ambayo inasababisha hali mbaya ya afya na pia wakati ambapo mtu ni mja mzito saa zingine huwa anaavya mimba. Kwa hivyo, wakati ambapo sheria hii tunayoitengeneza, ni vizuri Serikali itilie hili jambo maanani na kuharamisha tendo hili. Kwa hivyo, yule ambaye anatekeleza tendo hili aweze kuchukuliwa hatua kali sababu wakati ambapo tendo hili linamfanyikia yule mtoto wa kike, wengi huacha shule kwa sababu ya jambo hili. Vile vile wakati ambapo unapitia mahali unasikia watu wakizungumza, wakati mwingine unakosa raha ya kukaa na wao kwa ajili ya mambo ambayo wanayasema halafu wanajitenga kwa kufikiri kuwa wanaonewa. Kwa hivyo, ni vizuri katika zile jamii ambazo zinaendelea kutekeleza haya mambo, Wizara ya Jinsia ichukue nafasi hii kuelimisha zile jamii ili waweze kuyashika na kujua ya kwamba wakati wanatekeleza tendo hili, yule ambaye anatendewa anaweza umia sana . Hii ni kwa sababu tumesikia madaktari hapa wakisema kwamba wakati wa hedhi, damu inarudi ndani ya tumbo na kuharibu nyumba ya mtoto . Hili ni jambo ambalo tunafaa kulichukulia maanani sana. Wakati ambapo jambo kama hili linatekelezwa kule mashinani, kule ambako The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}