GET /api/v0.1/hansard/entries/1031413/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1031413,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1031413/?format=api",
"text_counter": 368,
"type": "speech",
"speaker_name": "Changamwe, ODM",
"speaker_title": "Hon. Omar Mwinyi",
"speaker": {
"id": 1345,
"legal_name": "Omar Mwinyi Shimbwa",
"slug": "omar-mwinyi-shimbwa"
},
"content": " Asante sana Naibu Spika wa Muda. Nasimama pia kuunga mkono mapendekezo ambayo Mwenyekiti wa Kamati yetu ya Uchukuzi ameleta mbele ya Bunge hili kuhusu Ripoti ya matumizi ya Standard Gauge Railway (SGR) katika taifa letu la Kenya. Mapendekezo ambayo yamekuja mbele ya Bunge hili ni kutokana na hali ambayo ilitokea na mtafaruku uliopatikana baada ya Serikali kushurutisha kuwa makasha na mizigo yote yabebwe na SGR. Jambo moja ambalo tumejifunza katika mtafaruku huu ni kuwa Serikali na raia wake wakifanya kazi pamoja, matatizo makubwa yanaweza kusuluhishwa bila kuwa na vurugu. Pia, imetuonyesha kuwa ni vizuri kuwa na miradi mikubwa kama hii ya SGR. Lakini, kabla haijatekelezwa, pengine watu washirikishwe na watoe maoni yao ili inapotekelezwa, watu wote washatoa mawazo yao na kuondoa zile hofu ambazo zingeleta mtafaruku siku za baadaye. Hiyo imeonekana wazi. Baada ya watu kutoa maoni, kukawa na masikizano. Jambo lingine ni kwamba Ripoti hii imewafanya Wabunge kufikiria kitaifa. Haikupendeza kuwa ilisemekana kuwa mambo haya yanadhuru sehemu za Pwani peke yake. The coastal regionis part of the nation . Ikiwa tatizo lagusa sehemu moja, latakiwa liguse nchi nzima. Sisi ni Wabunge The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}