GET /api/v0.1/hansard/entries/1031414/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1031414,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1031414/?format=api",
"text_counter": 369,
"type": "speech",
"speaker_name": "Changamwe, ODM",
"speaker_title": "Hon. Omar Mwinyi",
"speaker": {
"id": 1345,
"legal_name": "Omar Mwinyi Shimbwa",
"slug": "omar-mwinyi-shimbwa"
},
"content": "wakitaifa. Nilifurahishwa kuwa ingawaje ilikuja polepole, mwishowe tulipata usaidizi kwa sababu SGR ingeathiri sehemu kubwa sana ya nchi yetu. Si Pwani peke yake. Kando ya vile alivyoeleza Mwenyekiti wetu, tuliona kuwa katika usafirishaji wa haya makasha, badala ya kasha kuletwa mpaka Nairobi, ilikuwa kuna wale ambao wanachukua makasha hayo nakuyaregeza kwenye Port . Kwa sababu ya kuzuia msongamano kule Port, hao walikuwa na ahadi zao wakiwekeza. Baadaye, meli ikiwa tayari, wanayachukuwa na kuyaweka ndani ya meli na kuyapeleka ambako wanayapeleka. Hapo kulikuwa kuna nafasi nyingi za kazi zilizotokea kutokana na hali kama hii tunayozungumzia. Ilipokuwa ni lazima SGR ibebe mizigo hiyo na baadaye iregeshe, ikawa kuwa kila mtu atafutwa kazi kwa sababu huwezi kumlipa mfanyakazi ambaye hafanyi kazi nawe hupati pesa pia. Tumejifunza ni lazima tutumie hizi universities zetu kufanya utafiti katika mambo yote ambayo tunataka kufanya kama nchi. Vile vile, kila jambo linalofanywa lihusishe raia kwa ukubwa na upana kwa sababu ni raia ndio watakaoathirika ama watakaotumia zile services . SGR inakuja na kubeba watu lakini inawaangusha katika zile sehemu za Syokimau. Mtu anapaswa apande teksi aje mpaka mjini. Ulimwenguni mzima, huwa tunaona train services zinaishia ndani ya mji. Mtu anashuka na kutembea kwa mguu hadi ofisini. Kwa hayo machache, naunga mkono mapendekezo hayo na kuomba ndugu zangu pia waunge mkono."
}