GET /api/v0.1/hansard/entries/1031426/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1031426,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1031426/?format=api",
    "text_counter": 381,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Mishi Mboko",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": " Asante sana, Bw. Spika kwa sababu Waswahili wanasema, bandu bandu humaliza gogo. Swala hili tulilizungumzia kwa muda mrefu sana, haswa sisi Wabunge wa kutoka sehemu ya Pwani. Na kila wakati tulipokuwa tukilizungumzia, lilikuwa linaleta tashwishi na hamasa nyingi haswa kule kwetu Pwani. Lakini, kama Serikali na Wakenya, tumeangalia swala hili na tukaamua tuwe na mazungumzo. Na kwa kuzungumza kwetu, tumeweza kupata suluhu; suluhu ambayo itakuwa inamwangazia Mkenya kule mashinani na pia kuzingatia mikakati ya Serikali, ile kwa Kiingereza tunasema symbiotic model ambayo kila mmoja katika wale washikadau watafaulu na maamuzi haya ambayo yamewekwa na Kamati ya Bunge ya Uchukuzi. Nataka nishukuru sana kwamba hivi sasa wachukuzi walio na shehena zao katika Bandari ya Mombasa wataweza kutumia njia ambayo wameiona ni sawa kubebea zile shehena za mizigo. Iwapo unataka kutumia SGR, utaitumia na utajua malipo yake ni yepi; na iwapo umeamua kutumia uchukuzi wa barabarani, utautumia na utajua malipo yake ni gani. Basi, kukiwa na mipaka kama hiyo ile migogoro, zile sintofahamu, zile kashfa, mambo mengi na siasa duni zitakuwa zimezibwa katika kaburi la sahau. Nataka nizungumzie pia jambo ambalo limezungumziwa ambapo mtu atakuwa na uhuru wa kutafuta yule agent ambaye ako na leseni na anatambulika kisheria ili akutolee mizigo yako kutoka Bandari ya Mombasa. Sio wakati ule ambao tulikuwa tunashurutishwa ama kulazimishwa kutumia SGR na mikakati mingi sana iliyokuwa imewekwa. Kwa hivyo, hivi sasa, mtu atakuwa na uhuru. Utakuwa huna haja tena ya kuponda Serikali ama kuzungumza jambo lolote baya kuhusu Serikali. Jambo hili limezindua maneno mengi sana kwa sababu watu wamekuwa wakisema kwamba pengine SGR imeletwa ili iweze kufaidisha sehemu nyingine na kuua chumi za sehemu nyingine. Ndugu Mhe. Makau amesema kwamba njia yote kutoka Mombasa hadi Nairobi si watu wa Pwani pekee bali hata sehemu za Ukambani, uchumi ulikuwa umedorora, na ilikuwa ni shida sana kwa akina mama kufanya biashara ndogo ndogo katika barabara kuu. Wote walikaa majumbani na kukosa kupata mapato ambayo walikuwa wakipata kwenye biashara kama zile. Jambo kama hili ambalo sasa tumefanyia maamuzi kupitia Kamati ya Bunge ya Uchukuzi, ni jambo ambalo litaregesha ile ari ya sehemu hizi ambazo zilikuwa zina issues of logistics ama ambazo zilikuwa zinahusiana na mambo ya Bandari, kubeba mizigo na kupeleka sehemu tofauti. Vile vile, jambo ambalo amezungumizia tunaloliita ‘ last mile connectivity’ ambapo kama mtu anaweza kuzidisha barabara ama kurefusha ifikie mpaka mahali ambapo anataka shehena zake za mizigo zifike, pia amepewa uhuru wa kuweza kufuatilia na kufanya hivo. Kwa hivo, hii inamaana kwamba Serikali sasa imefungulia Wakenya walio na mizigo yao kutoka Bandari ya Mombasa na kupeleka sehemu yoyote nchini, wafanye biashara. Bwana Naibu Spika wa Muda, nashukuru sana na nasema kuwa kama Wakenya, mfumo huo wa kuzungumza, kusikizana na kuweza kufanya maamuzi ambayo yataweza kusaidia Mkenya, ni mfumo bora. Mambo mengine ya fujo, fitina na siasa duni hayatasaidia Kenya. Asante Bwana Spika."
}