GET /api/v0.1/hansard/entries/1031429/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1031429,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1031429/?format=api",
    "text_counter": 384,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Asante sana, Bwana Naibu Spika wa Muda. Historia leo imeweza kuandikwa. Tarehe 6 Agosti 2019, hili jambo lilipoanza, niliweza kuliuliza katika Bunge hili na likaleta sintofahamu na watu wakawa ni wenye kuzungumza ndani ya Bunge na wengine nje ya Bunge. Hatimaye, sheria zinatungwa na kutekelezwa katika Bunge hili. Sisi sote tumeweza kuwajibika na kupigiwa kura kwa sababu ya kutunga zile sheria, sio kwa kupiga porojo mitaani peke yake. Ilipofika tarehe 2 Juni 2020, hii Hoja iliregeshwa tena na nakumbuka niliweza kufuatilia katika Bunge hili na ndugu yangu, Mwenyekiti wa Kamati, akaleta jawabu ambalo sikufurahia. Tarehe 25 Juni 2020 nikaliuliza tena. Ndipo Mhe Spika akatoa amri ya kuwa ni lazima kuwe na kikao maluum cha kutafuta suluhisho la kudumu la masuala hayo. Nawaeleza kuwa tufahamikiane kuwa katika yale yaliyokubalika, kwanza ni kuwa kila mwenye mali awe na uhuru wa kuchagua njia yoyote anayoitaka kusafirisha bidhaa zake."
}