GET /api/v0.1/hansard/entries/1031434/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1031434,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1031434/?format=api",
"text_counter": 389,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mvita, ODM",
"speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Tulisema ni sawa ikiwa SGR inaona inatatizo la kupeleka mizigo kutoka yadi yao mpaka katika sehemu za wenyebiashara, ni sawa wazungumze na washikadau ambao ni wasafirishaji wakubaliane nao kuwa mizigo ikiingia, mtu ana hiari ya kutumia njia anayetaka ili mizigo ifike katika yadi yake. Zamani kazi za clearing and forwarding zilikuwa zimejaa Mombasa. Leo kwa sababu ya amri hii, biashara zote za clearing and forwarding zimeenda kwingine. Lakini tunakubaliana na nashukuru kuwa mtu awe na hiari ya kuchagua Container Freight Station anayoitaka na aweze kuwa na hiari ya kuchagua kampuni ambayo anataka."
}