GET /api/v0.1/hansard/entries/1031438/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1031438,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1031438/?format=api",
    "text_counter": 393,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": " Asante sana Naibu Spika wa Muda. Nilikuwa namalizia kwa kusema kuwa namshukuru Mwenyekiti na Wanakamati. Tulipoanza jambo hili kulikuwa na mvutano na bugudha sana. Nawasihi ndugu zangu wanaopendelea “ bonga points ” za mitaani kwa kuzungumza tu na kutoa kashfa ambazo hazina ukweli, kuwa leo pengine iwe funzo tunawapa jinsi sheria zinatungwa. Tumefaulu leo na nina imani kila mmoja amekubaliana na kauli yetu kuwa ni lazima SGR isiwe ya kulazimishiwa mtu bali iwe hiari kwa sababu wanaona inafaa."
}