GET /api/v0.1/hansard/entries/1032065/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1032065,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1032065/?format=api",
    "text_counter": 357,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Spika wa Muda. Nitazungumza kwa muda mfupi ili nimwachie dadangu dakika kwa vile naona amekusukuma hapo nyuma. Nimeangalia vizuri na kweli kunayo mazuri mengi ndani ya Arifa ya Rais ambayo ametoa hapa Bungeni. Kwa kweli alianza kabisa na wimbo wa taifa. Najivunia kwamba wimbo wa taifa hakika ulipatikana upande wangu huko Tana River. Mzee ambaye aliweza kuutunga wimbo huo alikufa tu miezi miwili iliyopita huko Makere ya Gwano. Kwa kweli BBI ni Ripoti kubwa ambayo ina mengi mazuri ndani, lakini nasi tuko na mengi ya kuweza kuweka kwenye hiyo BBI. Tungependa kama kuna fursa, mambo yetu ambayo ni muhimu yawekwe ndani ya hiyo Ripoti ya BBI. Tukipewa hiyo nafasi hatuna lazima ya kuipinga na tunaweza kuiunga mkono. Lakini kwa wakati huu kuna mengi ambayo iko nje ya BBI. Bw. Spika wa Muda, unaelewa vizuri ya kwamba, Rais wetu alizindua lugha ya Kiswahili tukiwa pale nje ili iweze kuongelewa katika Bunge zote tatu; Bunge la Kitaifa, Seneti pamoja na Bunge za Kaunti na nakala zote ziweze kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Hapo mbeleni, ningependa Arifa ya Rais iweze kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili ili tuweze kufahamu vizuri na kukuza lugha ya Kiswahili. Kwa mambo ya ardhi, sisi wengine tunawakilisha ardhi ambayo ni kubwa ambayo watu wake ni wachache. Mambo hayo yakiwekwa katika hiyo Ripoti ya BBI, sisi tutaweza kuiunga mkono. Ninaunga mkono. Asante."
}