GET /api/v0.1/hansard/entries/1032356/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1032356,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1032356/?format=api",
"text_counter": 265,
"type": "speech",
"speaker_name": "Lamu CWR, JP",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Ruweida Obo",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": " Asante Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii nichangia Ripoti hii ya Maeneo Maalum ya Kiuchumi. Mwanzo ningependa kuipongeza Kamati, Mwenyekiti akiwa Mhe. Kamket, na pia kuiunga mkono. Mashiriki ya umma hapa Kenya ni muhimu sana katika maendeleo endelevu. Hii ni kwa sababu unapata kujua wanaoishi mashinani au wataalamu. Utapata kuwasikiliza na mambo yao yawekwe kwenye ripoti. Kama hakuna ushiriki wa umma ama public participation basi si sawa. Ni muhimu hawa wataalamu wakiandika hizi ripoti waweze kuyajua yale mazingira. Wasiwe watu wa kukaa kwenye chumba cha bodi na kujiandikia mambo ambayo hawaelewi. Kwa mfano, huko Lamu wakitaka kujua maeneo maalum ya kiuchumi, itabidi wajue mazingira kwa sababu sehemu zingine ziko na mazingira tofauti. Mwenyezi Mungu ameumba mazingira tofauti, kama Lamu ni visiwa. Wakati mwingine watu wanataka kupanga mambo ya Lamu. Wanaenda huko na kupanda maboti, wakifika kwenye vile visiwa wanasikia kizunguzungu. Sasa hawawezi kuandika ile ripoti The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}