GET /api/v0.1/hansard/entries/1032590/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1032590,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1032590/?format=api",
    "text_counter": 129,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Laikipia North, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Sara Korere",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "Nitazungumzia kuhusu virusi vya Korona. Tumeona kwamba Mhe. Rais amefanya mengi na yote ambayo anaweza. Pia, ninapongeza Bunge hili kwa sababu waliketi chini kwa dharura, haswa Kamati ya Bajeti na Kamati ya Afya. Lakini inasikitisha kwamba baada ya Wabunge kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kwamba Wakenya wako salama na sekta ya afya iko sawa, kuna wale ambao waliona nafasi ya kujitajirisha kwa kuiba fedha. Inahuzunisha sana kwamba tunavyozungumza sasa hivi, sio Wakenya wa kawaida peke yao wanaokufa; madaktari pia wanaangamia."
}